Join   AY.CO.TZ   

»   Ay » Highlights 

A.Y Na Mwana FA Kutoka Pamoja!!  


A.Y Na Mwana FA Kutoka Pamoja!! Ile album inayosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wa bongoflava ya A.Y na Mwana FA sasa inatarajiwa kudondoka sokoni wiki ijayo.Album hiyo inayokwenda kwa jina la HABARI NDIO HIYO imejawa na mawe ya kufa mtu kutoka kwa wakali hao wawili ambao wameshirikisha pia vichwa vingine vingine vikali katika game ya muziki.

 
 

Mzee wa Commercial Anyakua Tuzo ya Kisima!!!  


Mzee wa Commercial Anyakua Tuzo ya Kisima!!!Kile kinyanganyiro cha kutafuta washindi wa tuzo za Kisima nchini Kenya hatimae kilifikia tamati jumamosi iliyopita na kutoa washindi kwenye makundi mbalimbali yaliyokuwepo.

A.Y almaarufu kwa jina la Mzee wa Commercial alidhihirisha kuwa mwaka huu ni wake na kwa kuweza kuibuka na Tuzo ya VIDEO BORA KUTOKA TANZANIA 2007 kupitia mwimbo wake wa USIJARIBU.

Ingawa hakuweza kutokea katika tukio zima la utoaji wa tuzo za KISIMA kutokana na majukumu yasioweza kuzuilika ila amepokea kwa furaha sana na kuwashukuru wadau na wapenzi wa muziki popote walipo kwa kuweza kumsupport kwa nguvu zote mpaka akafanikiwa kuchukua tuzo hiyo.Alisikika akisema kuwa Nimefurahishwa sana na kushinda tuzo hizo sina cha kuwalipa washabiki wangu zaidi ya kusema asanteni sana na nawaahidi kuwatengenezea kazi kali zaidi siku zijazo.
 
 

A.Y Ndani ya Dubai  


Baada ya kufanya makamuzi ya kufa mtu katika One Mic Concert,tamasha la kusheherekea miaka mitano ya EATV mkali wa miondoko ya Bongo Flava A.Y a.k.a MZEE WA COMMERCIAL anajiandaa kwa makamuzi ya kufa mtu ndani ya TANZANIA na DUBAI -FALME ZA KIARABU,

Kwa mujibu wa ratiba yake ya shows aliyotoa kwa mwezi huu wa AUGUST tarehe 19/08/2007 Jumapili A.Y ataperform ndani ya Dar Es Salaam maeneo ya MLIMANI CITY UDSM ambapo MTV BASE watakuwa wanamtafuta mtangazaji chipukizi kutoka TANZANIA.Baada ya hapo Mzee wa Commercial atakwea pipa mpaka Mtwara mkoa aliozaliwa miaka hiyooo na kufanya show ya nguvu ndani ya ukumbi wa BLANTYRE tarehe 24/08/2007 Ijumaa.
 
 

A.Y Aipa Pongezi - EATV  


A.Y Aipa Pongezi - EATVAmbwene Yessayah (A.Y) msanii wa muziki wa kizazi kimya nchini,ametoa pongezi kwa kituo cha television cha EAST AFRICA (EATV) kwa kutimiza miaka mitano toka kuanzishwa kwake kituo hicho.A.Y alitoa pongezi hizo kupitia mtandao wake,kwa kusema kituo hicho kimeweza kuwakilisha vema muziki wa bongo na Afrka Mashariki kwa ujumla na kuweza kazi zao kutambulika na kujulikana zaidi katika bara la Afrika na sehemu nyingine za dunia.

A.Y alisema sababu mashabiki wameweza vilevile kutambua kazi na uwezo wa wasanii wao wa hapa nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kama vile Kenya,Uganda nk.
 
 

"Usijaribu" ya A.Y Kuwania Tuzo ya Kisima  





Ni msimu mwingine tena wa kustawi kwa matunda katika mti huu na kwa watanzania wote.Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yessayah a.k.a A.Y anaendelea kuwakilisha vema nchi yetu ya Tanzania .


 
 

A.Y Kumuunga Mkono Mh. Rais J.K Kikwete  


A.Y Kumuunga Mkono Mh. Rais J.K Kikwete
A.Y KUMUUNGA MKONO RAIS WA JAMUHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JAKAYA M. KIKWETE JUU YA KUPIGA VITA GONJWA LA HATARI LA UKIMWI.

Baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Ambwene Yessayah – A.Y,kuendelea na ziara yake katika miji na sehemu tofauti katika ramani Tanzania na nchi za jirani kama vile Kenya na Uganda nk.

Jana tarehe 11/07/2007,A.Y aliungana na wanamuziiki mbalimbali kama vile NATIVE DEEN kutoka Marekani.Tamasha hilo la wazi lililofanyika katika viwanja vya Leaders club ,likiwa limesheheni umati wa watu kutoka kona zote za kanda ya Dar eas Salaam,wasanii hao wakiwa wamebeba ujumbe huu “HIP HOP AGAINST AIDS”.
 
 

Sasa Makamuzi Yanaelekezwa Zanzibar  


Baada ya kupiga shows za kufa mtu katika miji ya Arusha,Nakuru-Kenya na Moshi weekend iliyopita sasa A.Y atachana maji na na kuibukia Zanzibar ambapo atashusha show kali katika TAMASHA LA MAJAHAZI tarehe 6 Ijumaa.

"Bro nimejipanga vya kutosha,pia ni heshima kubwa kwa watu wa ZIFF kunipa nafasi hiyo na nadhani wanakubaliana na kazi nayoifanya..na kwa mara ya kwanza watu wangu wa Zanzibar nitaimba nao “USIJARIBU”...Najua hawafagilii mambo ya kishamba au sio,waambie washkaji nakuja kufanya mambo makubwa wajitokeze kwa wingi ijumaa" alisema MZEE WA COMMERCIAL…
 
 

Tour Nyingine ya A.Y Inakaribia Kuanza  


Tour Nyingine ya A.Y Inakaribia Kuanza TOUR NYINGINE YA A.Y INAKARIBIA KUANZA!! Baada ya kuchukua tuzo ya mwimbo bora wa hip hop wa mwaka katika KILIMANJARO MUSIC AWARDS,Na hivi majuzi akajiengua katika kundi lake la zamani la EAST COAST.
A.Y anatarajia kufanya maonyesho kadhaa ndani na nje ya nchi.

Mialiko hiyo tofauti tofauti imetokana na kufanya vizuri kazi yake katika sehemu tofauti tofauti za ndani na nje ya nchi.

Jumamosi ya tarehe 16 June A.Y atawasha moto ndani ya UKONGA jijini Dar Es Salaam katika kinyang'anyiro cha kumtafuta MISS UKONGA 2007 katika ukumbi wa FREETIME RESORT, Baada ya hapo makamuzi yataamia jijini Arusha tarehe 23 na 24 June ambapo ataunganika na mwanadada BESTA, JUACALI na DNA "Mzee wa BANJUKA" kutoka nchi KENYA ndani ya ukumbi wa BLUE TRIPLE A.Najua wana wa A-TOWN wanasubiri kwa hamu huko.
 
 

Habari Maalum Kutoka Kwa A.Y  


Habari Maalum Kutoka Kwa A.Y Leo hii nina taarifa muhimu moja ambayo ningependa kupitia website hii iwafikie wanahabari, mashabiki wangu na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini na kwingineko duniani.

Kabla ya kutoa taarifa hiyo, nianze kuwashukuru ndugu waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali, mashabiki wa muziki na wadau wengine popote mlipo kwa mchango wenu kwangu na kwa wasanii wenzangu, mchango ambao umenifanya mimi kuwepo hapa leo kuweza kuzungumza ninayokusudia kufanya sasa.
 
 

A.Y - Naomba Kura Yako  


A.Y - Naomba Kura YakoHaya ni matunda yanayotokana na kufanya muziki mzuri.A.Y amepata nafasi ya kuingia katika kinyang'nyiro cha kugombea kupata ushindi katika tuzo za muziki Tanzania "KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2007".

Jinsi ya kumpigia kura ni kama ifwatavyo: KWA WENYE SIMU ZA MIKONONI (SMS): -Andika neno kili na ACHA NAFASI na andika nambari 114 -Kisha tuma sms kupitia namba 15522