Kutokana na muziki wa bongo flava kufanikiwa kupenya katika mipaka ya nchi za Afrika ya Mashariki; ambapo katika nchi kama Kenya,Uganda,Burundi na Rwanda muziki huo umetokea kupendwa mpaka kufunika mpaka nyimbo zingine za nchi hizo;sasa zinaonekana dalili za muziki huo kwenda mbali zaidi.
Msanii mmoja wapo ambae anahusika kuutangaza muziki huo ndani na nje ya nchi Ambwene Yessayah “A.Y” ameamua kuuchukua muziki huo na kuupeleka Afrika Magharibi kwa ajili ya kuutangaza zaidi.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini A.Y tarehe 16 mwezi November anatarajia kufanya uzinduzi wa iliyo katika mfumo wa video inayoelezea historia ya maisha yake ya kimuziki na maisha yake binafsi (Documentary).

