Kutokana na muziki wa bongo flava kufanikiwa kupenya katika mipaka ya nchi za Afrika ya Mashariki; ambapo katika nchi kama Kenya,Uganda,Burundi na Rwanda muziki huo umetokea kupendwa mpaka kufunika mpaka nyimbo zingine za nchi hizo;sasa zinaonekana dalili za muziki huo kwenda mbali zaidi.
Msanii mmoja wapo ambae anahusika kuutangaza muziki huo ndani na nje ya nchi Ambwene Yessayah “A.Y” ameamua kuuchukua muziki huo na kuupeleka Afrika Magharibi kwa ajili ya kuutangaza zaidi.
Sasa anatarajia kurekodi wimbo mmoja na P-Square kundi ambalo linatamba ndani na nje ya Afrika linaloundwa na wakali wawili kutoka Nigeria “Paul na Peter .A.Y amesema nia na malengo makubwa ni kuutangaza muziki wa bongo flava magharbi mwa Afrika.Pia kujitangaza kwake upande huo utafanya ujenga ushirikiano zaidi kati ya mashariki,magharibi na Afrika kwa ujumla.
Nilikutana na P-Square Kampala-Uganda wakati nikiwa kwenye tour huko na wao wakiwa wamekuja kwenye show ya Akon.Jamaa wako kamili sana ndio maana nimependa kufanya nao kazi,wameonyesha moyo wa kunitangaza nchini kwao pia waliniambia walikuwa wanapenda kazi zangu hata kabla ya kukutana nao kwa kuwa video zangu walikuwa wanaziona kupitia kituo cha Mtv Base.Kwa sasa tupo kwenye uandishi kabla hatujaingia studio ambayo tutarekodi.nitawajulisha kama tutafanyia Lagos,Dar au sehemu nyingine pamoja.Jina la wimbo pamoja na lini wimbo huo utatoka nitawajulisha pindi kila kitu kitapokuwa tayari ila utakuwa funika trust me!alisema A.Y


