Mtandao huu ulipata fursa ya kuongea na kila mtu A.Y alisema…wakazi wa sehemu zote walizopita walijitokeza kwa wingi kumpokea kwa shangwe na furaha kubwa mshindi wa jumba hilo la BBA kwani kitendo cha kushinda na kupita kuwashukuru watanzania wenzake kimewapa faraja kubwa kwao. Prof Jay pia naye alinasawa na mtandao huu akisema “hii ni kama karama Richard aliyepewa na mwenyezi Mungu,kwani ni washiriki wengi walioshiriki katika nchi tofauti,lakini katika hizo nchi wengi wao waliweza kumpigia kura mshiriki aliyewakilisha Tanzania na kuibuka kifua mbele na kuweza kupeperusha bendera yetu vema.Mimi kama heavy weigth mc wengi huniita hivyo nimefurahia sana kuona mambo yalivyokwenda vizuri hata wasanii tuliyokuwepo katika tour hii ya nikimaanisha mimi,Juma Nature na A.Y tulisababisha burudani kali kabisa,zile silaha(nyimbo) za zamani na mpya ziliwakilishwa vyema..alimalizia kwa kusema mtu mbili kama elfu mbili”.
Sir Nature na alipata fursa ya kuongea na mtandao huu alisema alifurahishwa sana na ziara hiyo na anaamini mwaka 2008 ni mwaka wa kazi na washabiki wasubiri mambo makubwa kutoka kwake.Pia mtandao huu uliweza kumshika Richard katika mgahawa wa Sub Way pale maeneo ya Shoppers Plaza Msasani akiwa ameongozana na mshirki mwenzake Code kutoka Malawi;
Richard alisema kwanza kabisa anamshukuru Mwenyezi Mungu,wazazi,mkewe Ricky,multi choice Tanzania,Bia ya Serengeti,Red Promotion na zaidi ziwaendee watanzania kwa pamoja wote walioweza kumpigia kura na hata wale wasioweza kwani kwa imani zao waliweza kumuombea kwa Mungu na kuibuka kidedea katika jumba la Big Brother Africa 2007.
Maonyesho mengine ya A.Y aliyoweza kuyafanya vizuri pia ni kama la Coco Beach tarehe 30 Desemba na onyesho lingine lililobeba watu wengi sana lililofanyika Korogwe-Tanga kwenye ukumbi wa Mamba Club.


