
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ambwene Yessayah (A.Y),anatarajia kufungua kampuni yake unayohusiana na burudani.Akifanya mahojiano kupitia mtandao huu..
Mwandishi: Mambo vp mzee wa commercial?
A.Y: Poa!
Mwandishi: A.Y mimi nilikuwa na mambo kadhaa ya kuongea na wewe kuhusiana na biashara yako ya kimuziki zaidi.
A.Y: Hakuna tatizo kaka endelea…tu
Mwandishi: A.Y upo kwenye hii fani muda mrefu sana na kusema ukweli kabisa wewe sasa ni mmoja kati ya wasanii waliochangia kuinua muziki huu,kuna tetesi kuwa una mpango wa kufungua kampuni?
A.Y: Ni kweli kabisa,na sasa ipo katika hatua za mwisho mwisho mwezi wa pili tarehe moja kazi itaanza rasmi namshukuru Mungu mambo yote yanaenda sawa.
Mwandishi: Je! Hiyo kampuni inahusika na nini zaidi na inaitwaje?
A.Y: Kampuni hii inahusika zaidi na maswala ya burudani zaidi na kuratibu kazi za wasanii na inaitwa Unity Entertaiment Company Limited.
Mwandishi: A.Y umesema inahusiana na burudani kivipi ningependa uwelezee wasomaji wetu kwa kifupi?
A.Y: Zaidi tumelenga kwa wasanii wa hapa nyumbani na nje ya nchi,kuna mapromota wengi wangependa kufanya kazi na wasanii tofauti,sasa unakuta mawasiliano hana,hvyo anakuja ofisi za Unity Entertainment.Co.ltd au anafanya mawasiliano na ofisi anaelezea msanii anayemuihitaji.Tunampatia kwa makubaliano ya kiofisi zaidi na yule msanii pia naye tunamsimamia kwa kila kitu mpaka malipo yake yote analipwa na mamboyanaenda sawa.
Pia kuwatafutia shows za nje ya nchi kwa wasanii wa hapa nyumbani na wasanii wa nje nina mawasiliano ya karibu sana nao hivyo nawatafutia shows za hapa nchini na vilevile wandaaji wa matamasha wa hapa nchini wakiwa wanahitaji wasanii wa nje wanaweza kufanya mawasiliano na kampuni ya Unity ivyo inahakiki kuwa wanapata wasanii husika.Pia inahusika katika kuandaa matamasha(events) tofauti.
Mwandishi: Nadhani A.Y hapo wasomaji utakuwa umewafungua akili juu ya kampuni yako,lengo la kufungua kampuni ni nini zaidi?
A.Y: Lengo ni kama kawaida ni kujikita zaidi kibiashara na kuongeza ajira kwa vijana wenzangu wa kitanzania.Kifupi ni kuongeza kipato kwa wote.
Mwandishi: Sasa hao wasanii ni wewe unazo tayari namba zao na wako wasanii wangapi?
A.Y: Nashuru Mungu nina uhusiano mzuri sana na wasanii wenzangu hapa nyumbani na nje ya hapa,zaidi katika swala kama hili tunakuwa tumeingia katika biashara zaidi.Sasa wasanii wapo tayari ni wamesajiliwa katika kampuni idadi yao ni kama 70 ambao tayari wapo chini ya Unity Enertaiment Co.Ltd.
Mwandishi: Unaweza kututajia majina yao?
A.Y: Wako wasanii wakubwa kwa wadogo kutoka Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda,South Africa na Nigeria kusema kweli ni wengi sana idadi ya watu 70 siwezi kuitaja kwa sasa.Kampuni ya Unity Entertaiment itafungua tovuti(website) ili kujua zaidi msanii gani anapatikana kupitia kampuni hiyo.
Mwandishi: Mzee wa Commercial umekaa kimya kirefu wewe kama wewe kutoa nyimbo,toka Usijaribu vipi hapo unasemaje?
A.Y: (anaangua kicheko)Hapana mzee nyimbo ni nyingi sana na sasa nimesharekodi nyimbo kadha kama project yangu binafsi na natarajia ku-shoot video zangu mpya na kazi zote inasimamiwa na Ogopa Dee Jayz kutoka Kenya.Na napendelea kazi zangu nizitoe katika ubora wa hali juu.
Mwandishi: Ubora huo unauzungumziaje?
A.Y: Ni kama natoa wimbo mpaka video nahakikisha unakaa mwaka mmoja mpaka miwili kama ilivyo Usijaribu na sasa.Mambo yanakuja zaidi ya Usijaribu,mashabiki wangu wakae tayari tu.
Mwandishi: Vipi album yenu wewe na Mwana FA?
AY: Album ipo mtaani nashukuru mashabiki wameipokea vizuri kabisa na baadhi ya nyimbo zilizopo hewani zinafanya vizuri sana nakopi zinatoka kweli..Ha ha habari ndio hiyo…!!
Mwandishi: (Swali la kizushi),vp shemeji amesalimika huko?
A.Y: (Anatabasamu) Hajambo,na yupo kwao ametulia.
Mwandishi: A.Y la mwisho ningependa kuwaambia nini wasomaji wa tovuti hii?
A.Y: Mimi nawashukuru sana kwa kupenda kazi zangu na watarajie zaidi kupata mambo mazuri kutoka kwa A.Y.Sababu muda wote nasikia harufu ya ankara…. (anaonyeshe noti)
Mwandishi: Asante sana,mzee wa commercial. Nakutakia mafanikio mema.
A.Y:Shukrani sana kwa wote.


