Leo tarehe 11 December kuanzia saa tatu usiku A.Y atakuwepo katika viwanja vya Carnival Jijini Nairobi katika uzinduzi wa album mbili za wanamuziki maarufu wa Kenya Amani na Nonini.
Mzee wa Commercial ambaye tangu kipindi cha nyuma mpaka sasa amezidi kufanya vizuri na kujizolea washabiki wengi zaidi nchini humo amepata mualiko huo maalum ambao unaambatana na mkesha wa siku ya Uhuru wa Kenya.
Makamuzi yaliyoandaliwa na A.Y kwa ajili ya usiku wa leo ni makubwa sana na kilichobakia ni kusubiri muda wa tukio.
Kama kawaida yetu tutawaletea habari na picha za yaliyojiri usiku wa leo.


