Umati mkubwa uliweza kujitokeza kwenye ukumbi wa maraha wa Club Maisha ulioko Oysterbay.Uzinduzi huo iliofana ulidhaminiwa na Str8 Muzik na kutayarishwa na Lips Entertainment uliweza kuwavutia washabiki wengi sana ambao walionyesha utulivu wa hali ya juu hali ambayo iliashiria kuwa ni jinsi gain wanaridhika na mpangilio mzima wa tukio zima la siku hiyo.
YALIYOJIRI: Ukumbi wa Maisha ulikuwa tofauti kabisa na vile ulivyozoeleka sku zote;ulionekana umebeba umati mkubwa wa mashabiki wa muziki ambao walifuatilia kwa ukaribu kila tukio lililokuwa linatokea.Mambo yalianza hivi;pazia la burudani lilifunguliwa na msanii mkali ajulikanae kwa jina la Bandago ambae aliweza kuwarusha watu kwa wimbo wake unaotamba ujulikanao kwa jina la “Jiachie”.Baada ya hapo alifuatia mkali mwingine wa bongoflava Oten ambae alikamua sana jiwe lake “Nicheki” lililotamba sana kipindi cha nyuma.ghafla aliibuka mkali mwingine Snare ambaye alikuwa kundi moja na A.Y kipindi cha nyuma nae pia aliweza kuwashika vilivyo washabiki kwa kitu chake kipya “Funguo iliyopotea” kinachotamba hivi sasa.
Ukumbi ulilipuka zaidi kwa mayowe baada ya kumuona B.I.N.A.M.U au Mwana FA mkali wa mashairi ambae bila ya kusita aliweza kuwarusha vilivyo kwa kibao chake “Binamu”.baada ya makamuzi hayo ya nguvu ndipo tukio moja kati ya matukio muhimu ya kihistoria liliiweza kufanyika.
Mtangazaji maarufu wa radio Clouds Fm “B-12” aliweza kuwaongoza watu kuona yale yaliyomo katika website ya A.Y.Tukio hilo liliweza kuwavutia sana watu waliofika siku hiyo.Baada ya uzunduzi huo wa tovuti ndipo yule mwanadada mkali wa kutawala jukwaa Besta aliposhuka jukwaani na madansa wake na kupagawisha watu vya kutosha.Burudani haikuishia hapo;baada ya Besta kumaliza mambo mazito jukwaani kulifanyika tukio lingine lililowavutia sana watu ambapo wanamitindo maarufu waliweza kupita jukwaani na kuonyesha mavazi ya “Commercial Wear”.
Baada ya maonyesho hayo ya mavazi mkali wa r n’ b kutoka Uganda Michael Ross aliweza kuwashika watu vilivyo kwa vile aliweza kulitawala jukwaa ipasavyo,haikuishia hapo mkali mwingine ndani na nje ya bongo mwana wa TMK Juma Nature aliweza kufanya yale washabiki wanayoyahitaji kwa kukamua mfululizo mawe yake makali.Makamuzi yalizidi kupamba moto pale mkali toka Kenya Juacali ambae aliweza kwenda sambamba na washabiki wake kwa nyimbo zake zinazotamba na kudhihirisha kuwa ndiye mfalme wa muziki wa Genge toka Kenya.
Kilele cha shangwe kilizidi kukaribia pale watu walipata fursa ya kuangalia kwa ufupi documentary ya A.Y ambayo ilionyesha maisha ya kimuziki na nje ya muziki ya A.Y ambayo mkanda wake utaanza kupatikana madukani siku chache zijazo.
Pazia la burudani lilifungwa na mhusika mkuu Mzee wa Commercial ambae alikamua vibao vyake tofauti vya zamani na vipya n kuwashika vilivyo washabiki wake waliojitokeza kwa wingi siku hiyo.Wakati A.Y akiendelea kukamua ghafla akaibuka malkia wa muziki wa kizazi kipya cha Kenya Amani na kuwafanya washabiki washangilie kwa nguvu sana na bila ya kupotza muda akakamua mwimbo wake unaotamba sana wa “Missing my babe” na kufanya ukumbi uzidi kurindima kwa mayowe ya furaha.Na baada ya Amani kufanya “sapraizi” hiyo ya aina yake akapanda tena Mwana FA na na ndipo Dj.Hermy B akaachia beat ya wimbo unaotabiriwa kuwa utafanya vizuri sana siku za mbeleni unaoitwa Habari ndio hiyo na kufanya watu waruke na kuimba sambamba na wasanii hao.
Chanzo chetu cha habari kimeelezwa kwamba A.Y akishirikiana na waandaaji wana mpango wa kuwapelekea burudani mikoa mingine kama ilivyotokea Club Maisha.Picha za tukio zima la siku hiyo zinapatikana katika GALLERY.CLICK GALLERY..
Big Up A.Y,Big Up Str8 Muzik,Big Up Lips Entertainment kwa kufanya onyesho zuri na lililofana


