Ile album inayosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wa bongoflava ya A.Y na Mwana FA sasa inatarajiwa kudondoka sokoni wiki ijayo.Album hiyo inayokwenda kwa jina la HABARI NDIO HIYO imejawa na mawe ya kufa mtu kutoka kwa wakali hao wawili ambao wameshirikisha pia vichwa vingine vingine vikali katika game ya muziki.Album hiyo ina nyimbo kumi ambazo ni ASUBUHI feat. Q CHIEF, NANGOJA AGEUKE,FUNGUA CHAMPAGNE,HABARI NDIO HIYO,UMEJUAJE? feat. LADY JD, BOUNCE feat. CHAMELEONE, USIJARIBU, BINAMU, KULA KWA MACHO feat. TALIA kutoka KENYA, WE GOOD feat. MANGWEA.Watayarishaji waliofanya mawe hayo ni pamoja na MARCO CHALI (MJ PRODUCTION), HERMY B, LAMAR (41 RECORDS), BOSIRE (JOHARI CLIFF-KENYA) na LUCAS (OGOPA DEE JAYS-KENYA).
Inasemekana kuwa hutajilaumu kununua wala kuforward wakati unaisikiliza album hiyo.Na habari zilizotufikia hivi punde zinasema A.Y na Mwana F.A wameshakamilisha kufanya video mbili ambazo ni ASUBUHI na HABARI NDIO HIYO kupitia kampuni inayofanya video kali ya VISUAL LAB.Kaa tayari kukamata kopi ya album hiyo pata picha MWANAFALSAFA na MZEE WA COMMERCIAL wakifanya kazi pamoja nini kinatokea.Tutawafikishia habari punde tu album hiyo ikidondoka mtaani…


