Join   AY.CO.TZ   

»   Ay » Highlights » A.Y na Prezzo Wazua Balaa Nairobi 

A.Y na Prezzo Wazua Balaa Nairobi


A.Y na Prezzo Wazua Balaa Nairobi

Ambwene Yessayah ambae washabiki wa muziki wanamfahamu kama A.Y-mzee wa commercial,wiki ya jana aliweza kufanya umati wa watu kubaki midomo wazi kwa kumpigia mayowe baada ya kuibuka ghafla “kisapraizi” bila washabiki kujua kama alikuwa maeneo hayo viwanja vya Carnivore jijini Nairobi-Kenya.

Hii litokea kwenye show kubwa iliyojulikana kama Smirnoff Riev Up Concert ambayo ni moja kati ya show kubwa zinazofanyika nchini humo.Ilkuwa hivi baada ya msanii mwenzake na swahiba wake Jackson Makini almaarufu kama CMB PREZZO kukamua vilivyo na kabla ya kumalizia makamuzi ndipo alipowaambia mashabiki kwamba amemleta mgeni.

Prezzo alisema “leo nimewaletea mgeni ambae hamjamtegemea na mtu atakayeweza kuotea basi nitampatia zawadi”,wakati huo A.Y alikuwa mbele ya jukwaa huku akiwa amejifunika uso mzima,mashabiki hao walijaribu kwa kila hali kutaka kumjua na kubahatisha kutaja majina ya wasanii tofauti.Na ndipo zoezi hilo kuwa gumu kwa mashabiki hao na hatimaye Prezzo kumruhusu A.Y kuvua vazi hilo la kininja na kusikika mayowe ya nguvu huku wanausalama wakipata wakati mgumu wa kuwazuia washabiki wasipande jukwaani.

Basi bila ya kukawia wakali hao wawili walianza kukamua vilivyo mwimbo wa Nipe Nikupe na ukumbi ukalipuka zaidi kwa shangwe za nguvu.
  Discuss
Hello Guest. Please register or login to view hidden text..
Related News
  • "Usiku wa Undani Wangu" Wafunika
  • Tour ya A.Y Kenya Yafunika
  • A.Y Aipa Pongezi - EATV
  • Mzee wa Commercial Anyakua Tuzo ya Kisima!!!
  • A.Y Kumuunga Mkono Mh. Rais J.K Kikwete
  • Share

    #1 Author: DeltMarat 4 November 2011 12:40

    #2 Author: SantexDep 6 December 2011 02:29


    --
    --

    Портал отличный, буду рекомендовать знакомым!

    ----------------------------------------------------
    отопительное оборудование aqualux duravit

        
    Members of Guest cannot leave comments.