Join   AY.CO.TZ   

»   Ay » Highlights » A.Y Ndani ya Dubai 

A.Y Ndani ya Dubai


Baada ya kufanya makamuzi ya kufa mtu katika One Mic Concert,tamasha la kusheherekea miaka mitano ya EATV mkali wa miondoko ya Bongo Flava A.Y a.k.a MZEE WA COMMERCIAL anajiandaa kwa makamuzi ya kufa mtu ndani ya TANZANIA na DUBAI -FALME ZA KIARABU,

Kwa mujibu wa ratiba yake ya shows aliyotoa kwa mwezi huu wa AUGUST tarehe 19/08/2007 Jumapili A.Y ataperform ndani ya Dar Es Salaam maeneo ya MLIMANI CITY UDSM ambapo MTV BASE watakuwa wanamtafuta mtangazaji chipukizi kutoka TANZANIA.Baada ya hapo Mzee wa Commercial atakwea pipa mpaka Mtwara mkoa aliozaliwa miaka hiyooo na kufanya show ya nguvu ndani ya ukumbi wa BLANTYRE tarehe 24/08/2007 Ijumaa.

Na hataishia hapo kwani baaada ya kazi zake kukubalika ndani ya Afrika Mashariki na Kati sasa nyimbo zake zimeweza kukata maji na kupokelewa kwa nguvu zote barani ASIA na hivyo wadau wa muziki ndani ya DUBAI wameweza kufikia nae maelewano na hivyo A.Y atakwea tena pipa na kushuka ndani ya Dubai na kufanya show kali na ya maana tarehe 30/08/2007 ndani ya ukumbi wa AL MASAH BALLROOM –SHERATON DEIRA akiambatana na wasanii wenzake kutoka nchi jirani ya Kenya kama vile MR.LENNY,AMANI,MIKE RUA na DJ.NIJO kutoka M.O.B DEEJAYS.

“Sehemu zote nilizowatajia kuwa nitafanya shows ni kuwa mambo yote yanakwenda sawa hivyo nipo katika matayarisho wa mwisho na baada ya hapo ni kufanya kazi ya nguvu kitofauti na kiutaalamu zaidi.Nataka watu watambue HII NI NAMBA NYINGINE KATIKA PERFORMANCE hivyo wajitokeze kwa wingi na kuruka sana nyimbo zangu.”

“Na kwa watu wa Dubai ambapo itakuwa ni mara yangu ya kwanza kufanya show huko.. nawataka ndugu zangu wote wa Afrika ya Mashariki na Kati wajitokeze kwa wingi kuparty na EAST AND CENTRAL AFRICAN FINEST WAO A.Y!!Hata walio jirani na Dubai wasafiri bwana na tufurahie pamoja na A.Y 30th of AUGUST,Nawaahidi show nzuri sana yenye nidhamu ya hali ya juu,tupige picha nyingi,pia nitawaletea DVD’S,CD’S pamoja na POSTERS ambazo zitauzwa kwa bei nafuu siku hiyo ya show.”

Hayo ndio maelezo yake aliyoyatoa kwenye vyombo vya habari wakati alipohitajika kutoa ratiba yake ya mwezi huu.Kwa vitendo zaidi unaweza kuclick kwenye GALLERY na kuona picha nyingi zilizoongezwa kwenye mtandao huu pamoja na poster ya show ya Dubai..
  Discuss
Hello Guest. Please register or login to view hidden text..
Related News
  • Tour Nyingine ya A.Y Inakaribia Kuanza
  • Sasa Makamuzi Yanaelekezwa Zanzibar
  • Mzee wa Commercial Anyakua Tuzo ya Kisima!!!
  • Ay Apania Kuwarusha Vikali Dodoma, Mbeya na Moro
  • A.Y Kufanya Kazi na P-Square
  • Share

    #1 Author: DeltMarat 6 November 2011 10:19


    --
    --

        

    #2 Author: coollerok5713 25 March 2012 15:59


    --
    --

    Всем привет! Нашел рабочий сервис просмотра гостей Вконтакте. Пользуйтесь, пока не прикрыли - http://vk-secrets.com

        
    Members of Guest cannot leave comments.