Join   AY.CO.TZ   

»   Ay » Highlights » Mzee wa Commercial Anyakua Tuzo ya Kisima!!! 

Mzee wa Commercial Anyakua Tuzo ya Kisima!!!


Mzee wa Commercial Anyakua Tuzo ya Kisima!!!Kile kinyanganyiro cha kutafuta washindi wa tuzo za Kisima nchini Kenya hatimae kilifikia tamati jumamosi iliyopita na kutoa washindi kwenye makundi mbalimbali yaliyokuwepo.

A.Y almaarufu kwa jina la Mzee wa Commercial alidhihirisha kuwa mwaka huu ni wake na kwa kuweza kuibuka na Tuzo ya VIDEO BORA KUTOKA TANZANIA 2007 kupitia mwimbo wake wa USIJARIBU.

Ingawa hakuweza kutokea katika tukio zima la utoaji wa tuzo za KISIMA kutokana na majukumu yasioweza kuzuilika ila amepokea kwa furaha sana na kuwashukuru wadau na wapenzi wa muziki popote walipo kwa kuweza kumsupport kwa nguvu zote mpaka akafanikiwa kuchukua tuzo hiyo.Alisikika akisema kuwa Nimefurahishwa sana na kushinda tuzo hizo sina cha kuwalipa washabiki wangu zaidi ya kusema asanteni sana na nawaahidi kuwatengenezea kazi kali zaidi siku zijazo.

Vilevile mtanzania mwingine aliyeweza kuibuka na tuzo nchiniKenya ni Matonya ambae alipata tuzo ya MWIMBO BORA KUTOKA TANZANIA kupitia mwimbo wake wa VAILETH.

Kwa habari zaidi ingia www.kisimaawards.co.ke

Na habari zilizotufikia punde zinasema kuwa watu wengi walijitokeza kwa wingi sana katika concert ziliyofanyika Dubai,Jinja na Entebbe.Tukianzia Dubai ambapo wasanii kama Mr. Lenny,Amani,Mike Rua wote kutoka Kenya na A.Y kutoka Tanzania waliweza kuwakoga nyoyo zao wapenzi wa muziki wa Dubai katika ukumbi wa Ballroom-Sheraton Deira mpaka washabiki wakaomba kampuni ya Hamilton Gulf inayoendeshwa na Mr.Hassan ambayo ni muandaaji mkuu wa show hiyo kuwa pindi ipitapo mwezi mtukufu wa Ramadhani waweze kulirudia tena show hiyo.Imeelezwa kuwa wasanii hao waliweza kukamua vilivyo pamoja kupiga picha na washabiki wao huku wengi wao wakionekana wakinunua cd's na dvd's zao na kubadilishana nao mawazo kwa ukaribu zaidi.

Taarifa ziliendelea kusema kuwa shows za Jinja na Entebbe nazo pia ziliweza kupata nyomi la kiutu uzima wakati msanii Bebe Cool wa Uganda alikuwa akizindua album yake amabapo wasanii mbalimbali wanaotamba ndani na nje ya Afrika Mashariki walidondoka ndani ya ardhi ya Museven na kukamua vilivyo.wasanii kama A.Y na DUDU BAYA kutoka Tanzania,CMB PREZZO na LONGOMBAS kutoka Kenya,MARLON ASHER Mzee wa GANJA PLANTER kutoka Jamaica pamoja na wasanii wakali wa Uganda kama BOBBY WINE,PETER MILES na wengine wengi waliwakilisha vilivyo.

Ukitaka kuona picha kibao za shows za DUBAI, JINJA na ENTEBBE click GALLERY kisha shuka chini utaona picha.
  Discuss
Hello Guest. Please register or login to view hidden text..
Related News
  • A.Y Ndani ya Dubai
  • Tour ya A.Y Kenya Yafunika
  • "Usijaribu" ya A.Y Kuwania Tuzo ya Kisima
  • Tour Nyingine ya A.Y Inakaribia Kuanza
  • A.Y Anyakua Tuzo ya Kilimanjaro
  • Share

    #2 Author: Illessigh 7 November 2011 01:26


    Illessigh
    --

        

    #3 Author: zordenisk 11 November 2011 00:33


    Vladimir
    Moskva

        
    Members of Guest cannot leave comments.