"Bro nimejipanga vya kutosha,pia ni heshima kubwa kwa watu wa ZIFF kunipa nafasi hiyo na nadhani wanakubaliana na kazi nayoifanya..na kwa mara ya kwanza watu wangu wa Zanzibar nitaimba nao “USIJARIBU”...Najua hawafagilii mambo ya kishamba au sio,waambie washkaji nakuja kufanya mambo makubwa wajitokeze kwa wingi ijumaa" alisema MZEE WA COMMERCIAL…
Na pia alitudokeza kuwa ataambatana na SQUAD yake kamili,DJ wake pamoja na backup wake."Ni kweli nitaambatana na Dj. wangu pamoja na back up wangu kuonyesha niko kamili kamili,siku moja kabla ya show tarehe 5 nitasheherekea siku yangu ya kuzaliwa kisiwani humo kisha kesho yake tarehe 6 ni makamuzi kwa kwenda mbele,lazima niwafurahishe mashabiki wangu..."
Kila la kheri kamanda kwa show na siku yako wa kuzaliwa..miaka mingapi lakini unatimiza?????...hahahaha
Baada ya kutoka Zanzibar tutawawekea picha za show zake za ARUSHA,MOSHI,NAKURU na ZANZIBAR.


