Ambwene Yessayah (A.Y) msanii wa muziki wa kizazi kimya nchini,ametoa pongezi kwa kituo cha television cha EAST AFRICA (EATV) kwa kutimiza miaka mitano toka kuanzishwa kwake kituo hicho.A.Y alitoa pongezi hizo kupitia mtandao wake,kwa kusema kituo hicho kimeweza kuwakilisha vema muziki wa bongo na Afrka Mashariki kwa ujumla na kuweza kazi zao kutambulika na kujulikana zaidi katika bara la Afrika na sehemu nyingine za dunia.A.Y alisema sababu mashabiki wameweza vilevile kutambua kazi na uwezo wa wasanii wao wa hapa nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kama vile Kenya,Uganda nk.
Pia aliwapa pongezi kwa kuwandaa tamasha kubwa ambalo linalokutanisha wasanii wakali kutoka Afrika Mashariki,ambao kimuziki nao wanafanya vema na kuwakilisha nchi zao vema.Alisema hii ni changamoto kwake yeye na hata wasanii wenzake wa hapa nyumbani.Kwanza yeye kama yeye kusimama jukwaa moja na wakali wenzake toka Kenya na Uganda.
A.Y anakumbuka mara ya mwisho hapa nyumbani ilikuwa ni katika uzinduzi wake na mkali mwenzake T.I.D katika “HISIA ZA BURUDANI”.Ndipo alipokuwa jukwaa moja na Prezzo,Tatto,Necessary Noise kutoka Kenya na Mourice Kirya toka Uganda. Kwa muda mrefu A.Y amekuwa wa kupanda mwewe na kutoa burudani na wasanii wa Afrika Mashariki na Kusini katika nchi zao.Hi inatokana na mialiko mingi anayoipata.
A.Y anarudi kusimama tena hapa nyumbani jukwaa moja na hao wakali toka nchi za Kenya na Uganda akikumbukia “HISIA ZA BURUDANI” pale Daimond Jubilee.Sasa ni pale katika viwanja vya Ledears Club ndipo atakapoonyesha vema uwakilishi wake kama anavyofanya aendako na kufanya mashabiki wa huko kumkubali kama vile anavyokubalika hapa nyumbani Tanzania.
A.Y ambaye bila shaka atafanya makamuzi na wasanii kama vile Jua cali (UTAKE ANTHEM),Prezzo (Nipe Nikupe),DNA,Nyota Ndogo toka Kenya na Bebe Cool,Obbession,Michael Ross toka Uganda na bila kusahau hapa nyumbani Tanzania Prof.Jay,Nako 2 Nako,Lady Jay Dee na Besta.
KWA PAMOJA NJOONI MUONE A.Y ANAVYOSABABISHA KWENYE STAGE..!!


