
A.Y KUMUUNGA MKONO RAIS WA JAMUHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JAKAYA M. KIKWETE JUU YA KUPIGA VITA GONJWA LA HATARI LA UKIMWI.
Baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Ambwene Yessayah – A.Y,kuendelea na ziara yake katika miji na sehemu tofauti katika ramani Tanzania na nchi za jirani kama vile Kenya na Uganda nk.
Jana tarehe 11/07/2007,A.Y aliungana na wanamuziiki mbalimbali kama vile NATIVE DEEN kutoka Marekani.Tamasha hilo la wazi lililofanyika katika viwanja vya Leaders club ,likiwa limesheheni umati wa watu kutoka kona zote za kanda ya Dar eas Salaam,wasanii hao wakiwa wamebeba ujumbe huu “HIP HOP AGAINST AIDS”.
A.Y akiongea na mtandao wake alisema “Nimefurahi kuona watu walivyojitokeza kwa wingi na kupata ujumbe na burudani kwa wakati mmoja,naomba matamasha kama haya yafanyike mara kwa mara ili kuwahamasisha na kuelimisha watu .Namuunga mkono mh. Rais wetu kwa kusema kuwa TANZANIA BILA UKIMWI,INAWEZEKANA.Pia Nimefurahishwa na wasani wezangu wamejitokeza kwa wingi na kuunga mkono kampeni hiyo.” .Basi hayo ndiyo machache msanii alipata fursa ya kuzungumza na mtandao huu.


