Ni msimu mwingine tena wa kustawi kwa matunda katika mti huu na kwa watanzania wote.Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yessayah a.k.a A.Y anaendelea kuwakilisha vema nchi yetu ya Tanzania .
Kwa mara nyingine tena amechaguliwa katika kinyang’anyiro cha tuzo za muziki za nchini Kenya zijulikanazo kama KISIMA MUSIC AWARDS.A.Y ambaye anaendelea kutamba na mwimbo wake wa “USIJARIBU” ukiwa umebeba ujumbe mzito wa kuelimisha na bila shaka mengine hutokea katika jamii yetu.
A.Y amechaguliwa kuingia katika categories mbili tofauti ambazo ni VIDEO BORA KUTOKA TANZANIA na WIMBO BORA KUTOKA TANZANIA. A.Y aliongea na mtandao wake alisema “imenipa moyo sana kuona kazi zangu zinazidi kukubalika kila sehemu.
Kama kawaida watu wangu twendeni bega kwa bega katika kunipigia kura mpaka nikamate tuzo ya KISIMA kama vile mlivyonisupport kwenye KILI MUSIC AWARDS mpaka nikachukua TUZO YA WIMBO BORA WA HIP HOP WA MWAKA 2006-2007.Nawategemea sana ndugu zangu”.
Ili kuleta shangwe na furaha kwa watanzania tumpigie kura kwa wingi A.Y.Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea website ya waandaaji www.kisimaawards.co.ke


