Join   AY.CO.TZ   

»   Ay » Highlights » Tour Nyingine ya A.Y Inakaribia Kuanza 

Tour Nyingine ya A.Y Inakaribia Kuanza


Tour Nyingine ya A.Y Inakaribia KuanzaTOUR NYINGINE YA A.Y INAKARIBIA KUANZA!! Baada ya kuchukua tuzo ya mwimbo bora wa hip hop wa mwaka katika KILIMANJARO MUSIC AWARDS,Na hivi majuzi akajiengua katika kundi lake la zamani la EAST COAST..A.Y anatarajia kufanya maonyesho kadhaa ndani na nje ya nchi.Mialiko hiyo tofauti tofauti imetokana na kufanya vizuri kazi yake katika sehemu tofauti tofauti za ndani na nje ya nchi.

Jumamosi ya tarehe 16 June A.Y atawasha moto ndani ya UKONGA jijini Dar Es Salaam katika kinyang'anyiro cha kumtafuta MISS UKONGA 2007 katika ukumbi wa FREETIME RESORT,Baada ya hapo makamuzi yataamia jijini Arusha tarehe 23 na 24 June ambapo ataunganika na mwanadada BESTA,JUACALI na DNA "Mzee wa BANJUKA" kutoka nchi KENYA ndani ya ukumbi wa BLUE TRIPLE A.Najua wana wa A-TOWN wanasubiri kwa hamu huko.

Haitaishia hapo A.Y atavuka mipaka ya nchi yake mpaka nchini KENYA ndani ya Jiji la NAKURU ambapo kazi zake zinakubalika sana na kwa mara ya kwanza ndani ya jiji hilo tarehe 30 ya June atashika mic na kuwarusha washabiki wake ndani ya ukumbi wa COCO SAVANAH.Kisha atageuza mpaka mkoani KILIMANJARO tarehe 1 July ambapo ataunganika na washindi wenzake wa KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2007 na kufanya show kali mkoani humo.

Ili kudhihirisha kuwa kazi zake zinahitajika pande zote A.Y atavuka bahari na kushuka mpaka visiwani ZANZIBAR ambapo atadondosha show ya nguvu pamoja na wasanii mbalimbali wakali wa nje na ndani ya bara la Africa katika lile TAMASHA KUBWA LA MAJAHAZI(ZIFF FESTIVAL)linalofanyika mara moja kwa mwaka!!HAUTAKIWI KUKOSA ..

Hatokomea hapo...MZEE WA COMMERCIAL atarudi Jijini Dar Es Salaam na kukwea pipa mpaka Shinyanga ambapo wale washindi wa TUZO za KILIMANJARO watafanya makamuzi ya kufa mtu katika mkoa huo tarehe 14 Julai Jumamosi.Kisha watadondoka ndani ya Jiji la Mwanza na kuwarusha sana watu wao wa huko tarehe 15 Julai Jumapili.

“Nimepanga kuwafurahisha washabiki wangu,hata wale ambao hawajawahi kuona shows zangu watakiri kuwa hii ni mashine nyingine isiyo na kelele,sana sana inafanya kazi ya uhakika tu,Tarajieni mengi mazuri kokote nitapopita najua watu wangu manisubiri kwa hamu.Msiache kunipa support ya nguvu” alisema A.Y

AMINIA MZEE WA COMMERCIAL FANYA MAMBO ZAIDI NA ZAIDI!!! Kwa maelezo zaidi ya ratiba ya shows zake bofya “click” katika EVENTS….Pamoja!
  Discuss
Hello Guest. Please register or login to view hidden text..
Related News
  • A.Y Ndani ya Dubai
  • Ay Apania Kuwarusha Vikali Dodoma, Mbeya na Moro
  • Sasa Makamuzi Yanaelekezwa Zanzibar
  • Tour ya A.Y Kenya Yafunika
  • AY KUKAMUA NDANI YA MOSCOW RUSSIA JUMAMOSI HII:
  • Share

    #2 Author: OksanaSeksi 6 December 2011 05:40


    --
    --

    В это время множество одиноких сердец по ту сторону экрана находятся в поиске знакомства с Вами. Вы в любой момент сможете присоединиться к нашей очень дружной и веселой компании, и найти собеседника по душе, понравившегося друга по интересам , а так же более близкого человека для личной встречи.www mylove ru сайт знакомствсайт секс знакомств регистрация бесплатнаялучшие сайты знакомств

        
    Members of Guest cannot leave comments.