Mchakamchaka ulianzia Voi siku ya ijumaa tarehe 4 May katika ukumbi wa Voi Railway Club ambapo A.Y alifunika vilivyo, siku ya pili ambayo ni jumamosi ya tarehe 5 May A.Y alikuwa ndani ya POOLBAR MOMBASA ambapo aliwarusha maelfu ya wakazi wa mji huo wa mwambao na watu kukubali kama Bongoflava inaenda pazuri, na funga kazi ikawa siku ya jumapili ambapo A.Y alijumuika na MATONYA katika jiji la Nairobi kwenye ukumbi wa Savooy mbapo wasanii hao waliwakilisha vya kutosha mbele ya maelfu ya washabiki wao, pamoja na hayo pia baadhi ya wasanii mbalimbali wakubwa wa Kenya walijitokeza kushow love katika onyesho ambao ni kama ABASS KUBUFF, FLEXX, JAGUAR pamoja na DNA a.k.a 'MZEE WA BANJUKA'..
Na vile haitoshi sasa watu wa KISUMU na NAKURU wanamuhitaji sana A.Y aende kufanya maonyesho maeneo hayo.
BIG UP BONGO FLAVA!!BIG UP MUZIKI WA AFRIKA MASHARIKI!!!!


