Hivi siku za karibuni ni miezi mitatu ya nyuma alipata kuchagua video 3 bora kutoka bara la Africa .Ambapo moja kati ya video hizo ni ya " MADEMU WATAFUTAJI " ya A.Y aliyoshirikisha Stan Boy.Akon hakuishia hapo tu,pia aliweza kuichagua na kuiweka katika documetary yake.
Na hivi siku za karibuni tu ,AKON alihojiwa katika kituo kimoja kikubwa cha tevisioni nchini Marekani kituo hicho hujulikana kama BLACK ENTERTAIMENT TELEVISION. Kituo hicho nikinahusika zaidi na wasanii wakubwa duniani kuongoza baadhi ya vipindi hususani muziki mfano Ice cube,Dr Dre nk.Akon naye alipata nafasi mbili ya kuhojiwa na kupanga Top Ten zake katika televisioni hiyo ya B.E.T.
Akon akaulizwa "Ni msanii gani Africa anaweza kuwika hapa duniani na kuwa kama wewe na vilevile anakuvutia katika muziki wake?" Akon akajibu na kusema " Aaah! aah! Africa,A.Y ni msanii atakayefwata baada ya mimi.
A.Y anatoka nchi moja bara la Africa inaitwa Tanzania".Pia aliweza kutoa sababu akisema " A.Y ni mbunifu,yupo kibishara (commercial),kwa kweli hata sina hata la kuongea zaidi,watu wajaribu kutafuta kazi zake nyingine pamoja mimi sina zote,hii niliyonayo inanivutia sana nataka kutafuta kazi zake zaidi,ndiyo kwanza nikamwambia anitumie biography yake pamoja na mashairi ya "Mademu watafutaji.." yakiwa katika lugha ya kiingereza".
Akon pia aliongoza kipindi cha TOP TEN B.E.T nyimbo ya msanii A.Y Mademu watafutaji.. alichagua kuwa namba 3. BASI HUU NDIYO MWANZO WA WATANZANIA KUPIGA HATUA KATIKA SANAA YA MUZIKI...


