» Ay » Videos
Video Mpya ya Mwana FA na A.Y Wiki Hii
Baada ya kufunika vilivyo katika Sauti za Busara Visiwani Zanzibar nyota wa bongo flava Mwana FA na A.Y wanatarajia kutoa video mpya wa wimbo unaoitwa “NANGOJA AGEUKE” .Wimbo huo ambao unapatikana katika album yao ambayo ipo mtaani inayoitwa “HABARI NDIO HIYO”.Wimbo huo uliotengenezwa na producer mkali “Hermy B” ambaye pia alitengeneza wimbo mwingine uitwao Habari ndio hiyo unaosumbua anga la muziki wa Afrika Mashariki .
“Video ya wimbo huo imefanyika hapa hapa Dar es Salaam na kampuni ya Ogopa Dj’s kutoka Kenya,video ni kali sana na tunategemea watu wataifurahia na kuburudika nayo…itatoka ijumaa hii kwa hiyo watu wakae karibu na runinga zao..”alikaririwa Mwana fa.
Picha za shooting ya video hiyo na za Sauti za Busara tutawawekea mapema iwezekanavyo.



