(Aha) (Aha) Umeshaisikia hii?
Kutoka kwa A.Y
Chorus.
(Yule) Nampenda sana jinsi alivyo (Yule)
Nampenda sana jinsi alivyo simple.
(Yule) Nampenda sana jinsi alivyo, nitafanyaje?
PATAMU HAPO
Verse I.
Anavyotabasamu ndipo anaponipa hamu,
Sura umbo lake basi lanipa wazimu,
Nataka kumfuata, Nahisi atakataa,
Naogopa akinimwaga, story zitazagaa.
Napenda miondoko yake, tabia yake.
Umaskini wangu utanifanya nisimpate.
Yule , anayesumbua akili yangu.
Yule, anayeumiza moyo wangu.
Najua hafahamu, najua hafahamu,
Moyoni mi nabaki na mawazo. Lakini
Verse II.
Tatizo hajui, Bila penzi lake maze sijitambui.
Mi nitafanyeje, Hata nikimuona mdomo unajaa mate
(no x 6)
Napomuonaa, pindi tukikutana. Iwe club, kapozi na rafiki zake.
Ua tabu, napofikiria ni vipi nimfuate.
Muda utafika napo ukweli ntamueleza.
Nakosa raha pale washkaji wakinicheka…
Sijitambui, nae hajui kama kwake nimefika…
Chorus.
(Yule) Nampenda sana jinsi alivyo (Yule)
Nampenda sana jinsi alivyo simple.
(Yule) Nampenda sana jinsi alivyo, nitafanyaje?
PATAMU HAPO
Bridge.
Anavutia/cha ajabu hajidai.
Nataka awe wangu tu, lakini kumwambia ndo siwezi.
Chorus.
(Yule) Nampenda sana jinsi alivyo (Yule)
Nampenda sana jinsi alivyo simple.
(Yule) Nampenda sana jinsi alivyo, nitafanyaje?
PATAMU HAPO
Written by: Ambwene Yessayah.
Produced by: Steve Jean.
Video by: Paparazzi Production.


